IQNA

12:46 - February 19, 2009
Habari ID: 1745972

Baraza la Uhusaino wa Uislamu na Ukristo laasisiwa Kuwait

Baraza la Uhusaino wa Uislamu na Ukristo limeasisiwa rasmi nchini Kuwait tarehe 17 Februari.

Sherehe za kuasisiwa rasmi baraza hilo zimehudhuriwa na Sayyid Muhammad Baqer Mehri, Imam wa Msikiti wa Imam Ali AS na Radhawi Ardakani, Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika eneo la Diwania nchini Kuwait.
Sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi waandamizi wa Kikristo wakiwemo Wakatololiki na Waorthodoxi na Kiisalmu wakiwemo Mashia na Masunni nchini Kuwait.
Akizungumza katika sherehe hizo Sayyid Muhammad Baqer Mehri, Imam wa Msikiti wa Imam Ali AS amesema, Uislamu na mafuqaha wa Kiisalmu wakiwemo Sheikh Mufid, Ayatullah Sistani, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Khamenei na baadhi ya Maraji wametoa miongozo ya kuamiliana na wafuasi wa dini nyinginezo. Ameongeza kuwa Uislamu unaheshimu dini zote za mbinguni.
Naye Askofu Mkuu wa Kanisa la Orthodox la Kuwait Bizol Anba Bijoui amezungumzia suala la kuimarika uhusiano baina ya wafuasi wa dini za Mwenyezi Mungu.
Zahir al-Hamid Katibu Mkuu wa Harakati ya Al Tawafuq al Islami amezungumza kuhusu kuasisiwa baraza hilo la uhusiano wa Kiisalmu na Kikristo nchini Kuwait.
Kwa upande wake Razawi Ardakani Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu amesema ofisi yake iko tayari kushirikiana na baraza hilo kwa lengo la kuimarisha uhusiano baina ya dini mbalimbali. 365536

captcha