IQNA

10:41 - February 21, 2009
Habari ID: 1746469

Madai ya kiburi ya Waziri wa Watoto na Usawa wa Norway: Hijabu ni dharau kwa mwanamke!

Katika matamshi ya kiburi na matusi dhidi ya Uislamu, Bi Karita Bekkemellem, Waziri wa Watoto na Usawa wa Norway amedai kwamba vazi la hijabu kwa wanawake wa Kiislamu ni dalili ya unyama na dharau kwa wanawake hao!

Gazeti la al-Watan la Saudi Arabia limeandika kuhusiana na suala hilo kwamba, katika kuhalalaisha matamshi yake ya aibu, waziri huyo amedai kwamba ametoa matamshi hayo kama alama ya kuwajibika kwake katika kuwaunga mkono wanawake ambao amedai wanadharauliwa kwa jina la dini.
Waziri huyo wa Norway ametoa matamshi hayo ya kuaibisha katika hali ambayo mwaka 2007 yeye mwenyewe alisema kwamba vazi hilo la stara kwa mwanamke wa Kiislamu si alama ya dharau kwake.
Katika kipindi cha wiki iliyopita, hijabu kwa polisi wa kike wa Kiislamu imezusha mvutano mkubwa nchini Norway. Licha ya kuwa serikali ya nchi hiyo haipingi hijabu kwa wanawake wa Kiislamu, lakini viongozi kadhaa wa nchi hiyo wanalichukulia vazi hilo kuwa jambo hasi lisilopaswa kupewa fursa ya kuenea katika jamii ya nchi hiyo. 366769
captcha