IQNA

9:07 - February 23, 2009
Habari ID: 1747423

Bahrain, mwenyeji wa kikao cha kimataifa cha uwekezaji wa Kiislamu

Kikao cha tano cha kimataifa cha mashirika na mifuko ya uwekezaji wa Kiislamu kimepangwa kufanyika mwezi Mei nchini Bahrain kwa udhamini wa Jumuiya ya Uwekezaji wa Kiislamu ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Bahrain BNA, kikao hicho cha siku mbili kitahudhuriwa na idadi kubwa ya wanabenki mashuhuri wa kimataifa na wataalamu wa masuala ya benki katika eneo la Mashariki ya Kati. Kikao hicho kinafanyika kwa uungaji mkono wa Benki Kuu ya Bahrain. Washiriki wa kikao hicho watachunguza njia za kurekebisha miundo ya mashirika na mifuko ya uwekezaji wa Kiislamu ili ioane na misingi na sheria za Kiislamu.
Kutumiwa teknolojia na mbinu mpya katika mifuko ya uwekezaji wa Kiislamu, kufahamu mabadiliko yanayotokea katika masoko ya Kiislamu na kimataifa na pia namna ya kusimamia utajiri na mali za mifuko ya uwekezaji wa Kiislamu katika ngazi za kimataifa ni malengo mengine ya kikao hicho.
Kuhusiana na suala hilo, Arif Muhammad al-Alawi, mkurugenzi mwandamizi wa Jumuiya ya Uwekezaji wa Kiislamu ya Bahrain amezungumzia mgogoro wa uchumi unaoukumba ulimwengu na kusema kuwa, licha ya kuwa benki za Kiislamu hazijaathirika sana na mgogoro huo, lakini haziweza kupuuza athari zake kwazo na kwa mifuko ya uwekezaji wa Kiislamu. 367665
captcha