Sheikh Yazbak ameyasema hayo katika mazungumzo yake na Ayatullah Zanjani na kuongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni miongoni mwa neema ambazo zinamlazimu mwanadamu kumshukuru Mola.
Amesema kuwa kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran Waislamu wa Kishia wa Lebanon walikuwa na hali ngumu na kwamba hali hiyo iliboreka baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu chini ya uongozi wa hayati Imam Khomeini.
Kwa upande wake Ayatullah Zanjani ambaye ni mmoja wa wanafunzi wa Imam Khomeini amesisitiza kuwa njia na malengo ya Imam yamependwa na kuungwa mkono na watu katika pembe mbalimbali za dunia. Amesema kuwa kuna udharura wa kutambua thamani ya Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran na kuyalinda kwa hali na mali. 367568