Kwa mujibu wa televisheni ya Raswid, idadi kubwa ya Waislamu hao ilijeruhiwa na kupelekwa kwa matibabu katika hospitali za az-Zahra, al-Answar na Mfalme Fahd za nchini Saudi Arabia. Ripoti zinasema kuwa, Waislamu hao walikuwa wamekusanyika katika msikiti huo mtakatifu kwa lengo la kufanya maombolezo ya kukumbuka kifo cha mtume Muhammad (saw) na Imam Hassan Mujtaba (as). Wakiwa katika hali hiyo ya mkusayiko, ghafla askari usalama wa Saudia waliwavamia, kuwapiga na kuwatukana, ambapo idadi kadhaa ya Waislamu hao ilijeruhiwa na wengine kutiwa nguvuni. Kati ya watu waliojeruhiwa wamo wanawake na watoto, ambapo hali ya baadhi yao imetangazwa kuwa mbaya sana.
Shambulio hilo la kigaidi la askari usalama wa Saudia dhidi ya Mashia si jipya. Siku chache zilizopita pia yaani siku ya Ijumaa, askari hao waliwashambulia Waislamu wa Kishia waliokuwa wamekwenda kuzuru makaburi ya Baqii ambapo watukufu na viongozi wa Kiislamu wamezikwa, na kuwatawanya na kisha kuwatia nguvuni watano miongoni mwao. 368981