IQNA

10:55 - February 28, 2009
Habari ID: 1749217

Human Rights Watch yalaani marufuku ya hijabu kwa walimu wa kike nchini Ujerumani

Shirika la kutetea haki za binadamu lenye makao makuu nchini Marekani Human Rights Watch, limetoa taarifa likilaani hatua ya serikali ya Ujerumani ya kupiga marufuku uvaaji wa vazi la hijabu kwa wanake walimu wa Kiislamu nchini humo na kusema kuwa jambo hilo ni ukiukaji wa wazi wa haki za wanawake.

Shirika hilo limeonya dhidi ya athari mbaya za jambo hilo na kusema kuwa, upasishwaji wa sheria hiyo unakiuka haki za kimsingi na kidini za wanawake na kuimarisha zaidi ubaguzi wa kijinsia nchini humo.
Taarifa ya shirika hilo inaendelea kusema kuwa, sheria za Ujerumani zimelenga makusudi hijabu na wanawake wa Kiislamu na kuwalazimisha kuchagua moja kati ya vazi hilo na kazi zao za kijamii.
Taarifa ya Human Rights Watch imesema, marufuku hiyo kwa vazi la hijabu ni dhulma na kosa la wazi na kuongeza kuwa, kupigwa marufuku vazi hilo katika jamii ya kidemokrasia ni jambo lisilokubalika kabisa.
Wanawake wa Kiislamu wanazuiwa kuvaa hijabu nchini Ujerumani katika hali ambayo wanawake wa Kikristo na Kiyahudi wameruhusiwa kuendelea kuvaa nembo zao za kidini kwa mujibu wa mafundisho ya dini zao. 369803
captcha