Wakati huohuo ametilia mkazo umuhimu wa kukomeshwa mapigano ya pande mbili za utawala haramu wa Israel na makundi ya mapambano ya Wapalestina.
Mfalme Abdullah ametaka hatua za lazima zichukuliwe kwa lengo la kufanikisha mazungumzo ya mapatano ya pande hizo na kuongeza kuwa, hiyo ndiyo njia pekee ya kumaliza ghasia katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.
Mfalme Abdallah ameyasema hayo katika mazungumzo yake na George Mitchell, mjumbe maalumu wa Marekani katika Mashariki ya Kati na kuitaka serikali ya Washington ichukue hatua madhubuti katika kuzipatanisha pande mbili za utawala wa Israel na Wapalestina ili kusaidia kurejesha amani katika Mashariki ya Kati.
Amesisitiza pia juu ya udharura wa wakazi wa Ukanda wa Gaza kudhaminiwa mahitaji yao ya kimsingi ikiwemo ya kunufaika na misaada ya dharura ya kimataifa inayozuia kuingizwa katika ukanda huo na utawala ghasibu wa Israel. 371367