IQNA

12:34 - March 08, 2009
Habari ID: 1753174

Zafa ya Waislamu Zambia kwa mnasaba wa maulidi ya Mtume (saw)

Waislamu wa madhehebu za Shia na Suni wamepanga kufanya zafa kwa pamoja mjini Lusaka kuadhimisha Wiki ya Umoja wa Kiislamu na kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (saw), jambo ambalo ni mara ya kwanza kabisa kushuhudiwa nchini humo.

Washiriki katika zafa hiyo watabeba mabango yenye maandishi ya aya za Qur'ani na hadithi za Mtume (saw) zinazohimiza amani, usawa na uadilifu wa kijamii.
Lengo la harakati hiyo ni kuwaelimisha wananchi wa Zambia sira ya Mtume wa Uislamu.
Zafa hiyo imeidhinishwa rasmi na serikali ya Zambia.
Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Zambia Sheikh Muhammad Asadi Muwahhid atahutubia zafa hiyo akizungumzia umuhimu wa umoja kati ya Waislamu. 373972


captcha