Msemaji wa Batalioni ya Quds Abu Ahmad amesema kuwa baada ya kushindwa katika vita vya siku 22 dhidi ya Ukanda wa Gaza, utawala ghasibu wa Israel unatumia mbinu za vita vya kisaikolojia na majigambo kwa shabaha ya kuhuisha upya uwezo wake wa kijeshi.
Abu Ahmad amesisitiza kuwa, harakati ya Jihad Islami haitanyamazia kimya jinai za Israel na mauaji ya umati dhidi ya watu wasiokuwa na hatia.
Utawala wa Kizayuni wa Israel umetishia kwamba utaanzisha mashambulizi mapya ya kijeshi dhidi ya eneo la Ukanda wa Gaza, wiki kadhaa sasa tangu baada ya kulishambulia kinyama eneo hilo la kuua kwa umati Wapalestina wasiopungua 1400. 374098