Viongozi mbalimbali wa mashirika na taasisi za serikali na zisizokuwa za serikali wameshiriki katika sherere hizo zilizosimamiwa na Muhammad Ghanushi, Waziri Mkuu wa Tunisia.
Sherehe hizo zilizoandaliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Nchi za Kiislamu Isesco pia zimehudhuriwa na shakhsia mbalimbali wa kijamii, kidini, wasomi na matabaka mbalimbali ya wananchi wa Tunisia na wawakilishi wa nchi za Kiislamu. Akizungumza kwa niaba ya Rais Zine el Abidin bin Ali wa Tunisia, Ghanushi amelishukuru shirika la Isesco kwa kuandaa sherehe hizo na kutoa historia fupi ya mji wa Qairawan katika kueneza Uislamu na urithi wa Kiislamu katika ulimwengu wa Kiislamu.
Awali at-Tuwaijri alikuwa ametoa hotuba akiisifu serikali ya Tunisia kutokana na uungaji mkono wake kwa shughuli za Kiislamu, kusaidia mashirika ya Kiislamu na kushiriki kwake katika mipango ya kueneza misimamo ya wastani ya kidini. Amesema kuwa lengo la kuandaliwa sherehe hizo ni kueneza ustaarabu wa Kiislamu na kudhihirisha sura halisi ya utamaduni huo kwa walimwengu. Mji wa Qairawan ulijengwa mwaka 670 milaadia na Uqba bin Nafi', mmoja wa makamanda wa jeshi la Kiislamu, mji ambao ulikuwa mashuhuri baadaye kama kituo cha kupangiwa na kutekelezewa vita vya Kiislamu barani Ulaya. Badaye mji huo ulitembelewa na wanafikra pamoja na wasomi wa Kiislamu kutoka katika miji mitakatifu ya Madina na Makka. 375310