IQNA

20:06 - March 31, 2009
Habari ID: 1759348

Chuo Kikuu cha Catalonia kutoa cheti cha kimataifa cha utafiti wa Kiislamu na Kiarabu

Chuo Kikuu majazi cha Catalonia huko Barcelona nchini Hispania kitatoa cheti cha kimataifa cha utafiti wa Kiislamu na Kiarabu.

Chuo kikuu hicho kisicho cha kiserikali ni chuo pekee majazi ulimwenguni ambacho kinazidi kuenea duniani kwa kutoa masomo ya Kiislamu kwa kutegemea wataalamu na wahadhiri 250. Kwa kuzingatia hamu kubwa ya watu wa Ulaya ya kutaka kujua lugha ya Kiarabu na masuala yanayohusiana na Uislamu, chuo kikuu hicho kimekuwa kikieneza shughuli zake kwa kasi kubwa katika nchi za bara hilo kwa kuwategemea wataalamu wake waliobebea katika uwanja huo. Mgogoro wa ukisasa, na sio wa kifedha tu, chuki dhidi ya Uislamu, jamii za Kiislamu katika nchi za Magharibi, uhajiri na utandawazi ni miongoni mwa sababu ambazo zimezipelekea jamii za Magharibi kutaka kupata masomo na kufanya utafiti zaidi kuhusiana na ulimwengu wa Kiislamu na Kiarabu.
Masuala ya kisiasa na kiusalama ambayo ndiyo changamoto kubwa zaidi ya ulimwengu wa Kiislamu ni baadhi ya mambo ambayo yamewapelekea wakuu wa chuo hicho kuanzisha masomo hayo ya Kiislamu na Kiarabu na kutoa cheti cha digri kwa wanachuo watakaohitimu masomo hayo. 381527
captcha