Kwa mujibu wa gazeti la Qatar la as-Sharq, mwanazuoni huyo wa Kishia amehalalisha takwa lake hilo kwa kusema, maadamu Tripoli haitawajibika vilivyo na kubainisha wazi njama ya kutekwa nyara Imam Musa Swadr, mwanazuoni mwingine mashuhuri wa nchi hiyo akiwa na wenzake katika ardhi ya Libya, Lebanon haipasi kutuma mwakilishi wa kuiwakilisha katika kikao hicho, ambacho kimepangwa kufanyika nchini humo mwaka ujao wa 2010.
Ameendelea kusema kuwa Libya inapasa kujieleza vyema kuhusiana na kutekwa nyara mwanazuoni huyo na wenzake walipokuwa safarini nchini humo mwaka 1978.
Wanazuoni wa Kishia nchini Lebanon wamekuwa wakimtuhumu Kanali Muammar Gaddafi kuwa ndiye aliyehusika na njama ya kumteka nyara mwanazuoni huyo mashuhuri wa Lebanon na wasaidizi wake, na mahakama moja ya nchi hiyo tayari imetoa hukumu ya kutiwa kwake nguvuni bila ya yeye kuhudhuria mahakamani. 382971