IQNA

16:05 - April 06, 2009
Habari ID: 1761146

Jamii ya kimataifa inapasa kuunga mkono utekelezaji wa sheria Ukanda wa Gaza

Mkurugenzi wa Wakala wa Umoja wa Mataifa wa Misaada kwa Wapalestina UNRWA amesema kuwa kuna udharura kwa jamii ya kimataifa kulisaidia eneo la Ukanda wa Gaza na kuhimiza utekelezaji wa sheria ili kuzuia mauaji ya raia katika eneo hilo katika siku zijazo.

John Ging amesema kuwa iwapo jamii ya kimataifa itaunga mkono na kusaidia utekeleza wa sheria katika Ukanda wa Gaza, kuna matumaini makubwa ya kuboreshwa hali ya eneo hilo la Palestina.
Ging ameelezea wasiwasi wake kuhusu hali mbaya ya kimaisha ya watu wa Gaza ambao hawawezi hata kumudu mahitaji yao ya awali na akasema kuwa hali ya eneo hilo imekuwa mbaya zaidi licha ya kupita miezi miwili sasa baada ya mashambulizi ya kijeshi ya Israel dhidi ya eneo hilo.
Mkurugenzi wa operesheni za misaada za UNRWA ametoa wito wa kufunguliwa kikamilfu vivuko vyote vya kuingia Ukanda wa Gaza na akaongeza kuwa, kazi ya kulijenga upya eneo hilo lililoharibiwa vibaya na mashambulizi ya Israel haitafanikiwa hadi pale wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu watakaporuhusiwa kuingia kwa uhuru huko Gaza.
Wakati wa mashambulizi ya kinyama ya siku 22 ya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wakazi wa Gaza, karibu Wapalestina 1500 waliuawa shahidi, 5300 kujeruhiwa na maelfu ya nyumba, shule, hospitali na misikiti kubomolewa. 383026

captcha