IQNA

Wito wa Umoja wa Mataifa wa kutumiwa mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu duniani

14:13 - April 07, 2009
Habari ID: 1761407
Joseph E. Stiglitz, mshindi wa tuzo ya Nobel katika masuala ya uchumi mwaka 2001 ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Wataalamu wa Masuala ya Mfumo wa Fedha na Kiuchumi Duniani ya Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa walimwengu wazingatie mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu.
Akiashiria mgogoro wa kiuchumi unaoendelea hivi sasa ulimwenguni, Stinglitz amebainisha ubora wa mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu na kusisitiza kwamba taasisi na shakhsia muhimu wa kimataifa akiwemo Papa Benedict XVI wamekuwa wakizingatia na kusisitiza kutekelezwa kwa mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu.
Amesema kuwa, ili kutatua mgogoro wa kiuchumi unaotawala duniani, nchi za Magharibi zinalazimika kutafuta njia mbalimbali za ufumbuzi na kwamba moja ya ufumbuzi huo ni kutekeleza mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu ambao umekuwa ukiimarika siku hadi siku.
Stiglitz amesema kuwa licha ya kuwepo matatizo chungu nzima katika kamisheni hiyo ya masuala ya kifedha, lakini wanachama wake wamekubaliana kwa sauti moja kwamba moja ya njia bora za ufumbuzi wa haraka wa mgogoro wa hivi sasa duniani ni kutekelezwa mfumo wa uchumi wa Kiislamu. 383544
captcha