IQNA

Viongozi wa Iran na Masheikh wa Vyuo vya Kiislamu watoa rambirambi kwa Ayatullah Sistani

16:40 - September 30, 2025
Habari ID: 3481306
IQNA – Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ametuma ujumbe wa rambirambi kwa kiongozi mkuu wa Kishia nchini Iraq, Ayatullah Ali al-Sistani, kufuatia kifo cha mke wake mpendwa.

“Natoa rambirambi zangu kwa msiba wa mke wako mtukufu, na naomba rehema na msamaha wa Mwenyezi Mungu kwa ajili yake,” alisema Ayatullah Khamenei katika ujumbe wake siku ya Jumatatu.

Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, Spika wa Bunge Mohammad Bagher Ghalibaf, pamoja na maulamaa wakuu na wasomi wa vyuo vya Kiislamu, akiwemo  Ayatullah Abdullah Javadi Amoli, pia walitoa taarifa za rambirambi kufuatia msiba huo.

Mke wa Ayatullah Sistani alifariki Jumapili jioni baada ya kuugua kwa muda. Mazishi yake yalifanyika siku ya Jumatatu na mwili wake ukazikwa katika Msikiti wa Sheikh Tusi.

4307821

Kishikizo: Ayatullah Sistani
captcha