IQNA

Haram Takatifu ya Qom kuandaa hafla ya kumbukumbu ya kifo cha viongozi wa Hizbullah

16:52 - September 30, 2025
Habari ID: 3481307
IQNA – Hafla maalum ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuuawa shahidi kwa viongozi wa harakati ya muqawama ya Hizbullah ya Lebanon imepangwa kufanyika wiki hii katika haram tukufu ya Hazrat Masoumeh (SA) huko Qom.

Katibu mkuu wa zamani wa Hezbullah, Sayyid Hassan Nasrallah, aliuawa shahidi tarehe 27 Septemba 2024 katika shambulizi la kigaidi la Israeli lililotokea katika kitongoji cha kusini mwa Beirut, likitumia mabomu ya kisasa yaliyotengenezwa Marekani.

Sayyid Hashem Safieddine, ambaye aliongoza Hezbollah kwa muda wa wiki moja baada ya kuuawa kwa Nasrallah, naye pia aliuawa shahidi pamoja na wenzake kadhaa katika shambulizi jingine la kigaidi la Israel katika vitongoji vya kusini mwa Beirut tarehe 3 Oktoba 2024.

Hafla ya kuwakumbuka mashahidi hao itafanyika katika Ukumbi wa Imam Khomeini (RA) ndani ya haram tukufu ya Qom siku ya Jumatano, baada ya sala za Magharibi na Isha.

Masheikh wakuu wa vyuo vya Kiislamu, wasomi wa kitaaluma, wageni wa kimataifa, familia za mashahidi, na makundi mbalimbali ya waumini wanatarajiwa kuhudhuria tukio hilo.

Sayed Hassan Nasrallah (R) and Sayed Hashem Safieddine (L)

Miongoni mwa taasisi zinazoshiriki katika maandalizi ya hafla hiyo ni Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu huko Qom, Usimamizi wa haram ya Hazrat Masoumeh (SA), Jumuiya ya Kimataifa ya  Kukaribisha Madhehebu za Kiislamu, Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa, Ofisi ya Uenezi wa Kiislamu ya Chuo cha Qom, Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu, Taasisi ya Al-Bayt, Jumuiya ya Al-Bayt Al-Alamiyah, na Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (AS).

3494804

captcha