Kwa mujibu wa tovuti ya Muhit, al-Masrawi amesema kuwa mbinu mpya kabisa imetumika katika uandishi wa Qur'ani hiyo na ubunifu mkubwa kutumika katika uandishi huo. Amesema visomo hivyo kumi na nne vimeandikwa kwa rangi tofauti na kwamba kila rangi inabainisha kanuni maalumu za usomaji wa Qur'ani kwa mbinu kumi na nne tofauti.
Ahmad al-Masrawi amesema wasomaji wenye ujuzi na wasio na ujuzi mkubwa kuhusiana na usomaji wa Qur'ani wanaweza kutambua na kufahamu kwa urahisi sheria za usomaji huo mara tu baada ya kutupia jicho maandishi hayo yaliyoandikwa kwa rangi na kwa mbinu kumi na nne tofauti, na hivyo kunufaika na mafundisho ya kitabu hicho cha wahyi.
Al-Masrawi amesema mwishoni kwamba, mambo mengi ambayo kwa kawaida huwa hayafafanuliwi yamebainishwa na kuwekwa wazi kwa msomaji kupitia mbinu hizo. 383654