IQNA

12:10 - April 09, 2009
Habari ID: 1762315

Isesco kushiriki katika kikao cha Maisha ya Mtume (saw) katika maandiko ya Marekani

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa nchi za Kiislamu Isesco litashiriki katika kikao cha kimataifa kitakachofanyika chini ya anwani ya Maisha ya Mtume (saw) katika Maandiko ya Marekani ambacho kimepangwa kufanyika tarehe 14 hadi 16 katika mji wa Fas Morocco.

Kikao hicho kitafanyika kwa udhamini wa Chuo cha Fasihi na Elimu ya Ubinadamu na Chuo Kikuu cha Sayyid Muhammad bin Abdallah kwa ushirikiano wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Dini ya Morocco na pia Isesco.
Wanafikra na wasomi kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu watashiriki katika kikao hicho na kubadilishana mawazo kuhusiana na historia na maandishi yanayohusiana na maisha ya Mtume Muhammad (Saw) katika mtazamo wa wataalamu wa Marekani wa masuala ya mashariki mwa Dunia na vilevile ya Uislamu.
Washiriki pia watachunguza jinsi shakhsia tukufu ya Mtume Muhammad (saw) inavyoakisiwa katika maandishi ya fasihi na kidini, vyombo vya habari, taasisi za utafiti na vilevile katika mashule ya Marekani. 384812
captcha