IQNA

21:27 - April 10, 2009
Habari ID: 1762750

Mkutano wa Muungano wa Jumuiya za Kiislamu waanza nchini Ufaransa

Mkutano wa kila mwaka wa Muungano wa Jumuiya za Kiislamu za Ufaransa umeanza kazi zake leo katika mji wa Bourget chini ya anwani ya "Dini katika jamii za kisasa, thamani za pamoja na sifa zinazopaswa kulindwa".

Taarifa iliyotolewa na Muungano wa Jumuiya za Kiislamu za Ufaransa (UOIF) imesema kuwa zaidi ya Waislamu laki moja na nusu wa Ufaransa na nchi nyingine jirani wanahudhuria mkutano huo.
Taarifa hiyo imesema kuwa katika zama za sasa dini ina nafasi muhimu katika maisha ya mtu binafsi na jamii na inabadili mtazamo wa watu kuhusu maisha na mauti.
Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imesisitiza kuwa dini inamuonyesha mwanadamu nafasi yake halisi katika dunia hii na kwa msingi huo mkutano huo ambao utajadili nafasi na mchango wa dini katika zama za sasa utapanua mtazamo wa washiriki kuhusu dini.
Masuala mengi yanayojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na utafiti wa kitiba, kutoa zawadi ya damu na viungo vya mwili na maudhui ya serikali zisizokuwa za kidini.
Vilevile washiriki watabadilishana mawazo kuhusu mchango wa familia, Uislamu na utaifa na nafasi ya dini katika jamii za kidemokrasia. 385627


captcha