Ibada hiyo ya dua katika misikiti yote ya Italia imefanyika kwa wito wa Imam wa msikitu mkuu wa Roma Sheikh Abdullah Radovan.
Sheikh Radovan amewataka pia Waislamu wa Italia kuwasaidia kwa hali na mali watu walioathirika na mtemtemeko huo.
Wakati huo huo Jumuiya ya Kiislamu ya eneo la L'Apuila na Muungano wa Jumuiya za Kiislamu za Italia zimetangaza kuwa ziko tayari kutuma misaada zaidi kwa waathirika wa mtetemeko huo wa ardhi. Hadi sasa jumuiya hizo za Kiislamu zimechukua hatua kadhaa kuwasaidia waathirika wa mtetemeko huo uliokuwa na nguvu ya 6.3 kwa kipimo cha Rishta.
Mtetemeko huo uliolikumba eneo la katikati mwa Italia umesababisha vifo vya watu wasiopungua 278 na kuwajeruhi wengine wengi. 385652