Wayahudi wenye misimamo mikali wamepanga kuwazuia Waislamau wa Palestina kuingia katika haram ya Nabi Ibrahim katika siku za Jumapili na Jumatatu ya wiki hii katika hatua ambayo imetambuliwa kuwa dhidi ya dini.
Mkurugenzi wa Wakfu wa eneo la al Khalil huko Palestina Zaid al Jaabari amelaani vikali hatua hiyo ya Wazayuni wa Israel na kutangaza kuwa ni katika harakati za utawala ghasibu za kulifanya eneo hilo tukufu kuwa la Kiyahudi.
Amesema kuwa haramu ya Nabi Ibrahimu ni milki ya Waislamu, na wasiokuwa wafuasi wa dini hiyo hawapaswi kutekeleza ibada zao katika eneo hilo.
Askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamekuwa wakiwazuia Waislamu wa Palestina kuingia katika haram ya Nabi Ibrahim katika minasaba na matukio mbalimbali. Hatua hiyo ilichukuliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1994.385744