IQNA

Maulamaa wa Afghanistan wasisitiza umuhimu wa kulinda utulivu

14:32 - April 12, 2009
Habari ID: 1763537
Mabaraza ya maulamaa wa Afghanistan yametoa ripoti yakimuunga mkono Rais Hamid Karzai wa nchi hiyo na kusisitiza juu ya udharura wa kulindwa utulivu na amani nchini humo.
Mabaraza ya maulamaa wa Kiislamu ya mikoa ya Konar, Kunduz na Harat yameunga mkono kubakia madarakani Rais Karzai hadi wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu.
Mwenyekiti wa Baraza la Maulamaa wa mkoa wa Konar amesema kuwa Uislamu ni dini ya amani na utulivu inayopinga ghasia na ukosefu wa amani katika jamii. Amesema kuwa baraza hilo linamuunga mkono Rais Hamid Karzai kwani halitaki kuona Afghanistan ikitumbukia tena katika mgogoro wa kisiasa.
Kipindi cha uongozi wa Rais Hamid Karzai wa Afghanistan kitaongezwa kwa miezi mitatu baada ya nchi hiyo kushindwa kutayarisha uchaguzi kwa kipindi kilichoainishwa kikatiba. 384048
captcha