Waziri huyo amesema kuwa hakuna mgongano wowote kati ya mtu kuwa Muislamu na wakati huohuo kuhudumu katika jeshi la Uingereza.
Akizungumza hivi karibuni katika hadhara ya askari jeshi wa Uingereza, ameashiria suala la Waislamu kutuhumiwa kuwa magaidi katika kipindi cha miaka iliyopita na kusema kuwa, kamwe Waislamu wachache wa Uingereza hawawezi kutuhumiwa kuwa wanahusika na vitendo vya ugaidi.
Waziri huyo alisema mwishoni kwamba, vitendo vya utumiaji mabavu na ugaidi ni masuala muhimu mno yanayopasa kupigwa vita kwa kila njia.
Waislamu wapatao 390 wanahudumu katika jeshi la Uingereza, na Muislamu wa kwanza aliingia katika jeshi hilo mwaka 2001. 386774