IQNA

16:12 - April 14, 2009
Habari ID: 1764948

Harakati ya Kiislamu ya Palestina kususia safari ya Papa huko Israel

Harakati ya Kiislamu ya Palestina imeamua kususia safari iliyopangwa kufanywa na Kiongozi wa Wakatoliki duniani Papa Benedict wa 16 katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Israel.

Harakti ya Kiislamu ya Palestina inayoongozwa na Sheikh Raid Salah imesema itasusia safari ya Papa Benedict huko Israel na katika Ukanda wa Gaza kwa sababu ya matamshi yake yaliyomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw).
Taarifa ya harakati hiyo imesema kuwa uhusiano wowote kati ya Waislamu na Wakristo unapaswa kujengeka juu ya misingi ya kuheshimiana na kushirikiana na kwamba Papa Benedict amekiuka msingi hiyo.
Taarifa ya Harakati ya Kiislamu katika ardhi za Palestina inayokaliwa kwa mabavu imesema kuwa Papa Benedict hajaomba radhi kwa maneno yake yaliyovunjia heshima matukufu ya Kiislamu.
Kiongozi wa Wakatoliki duniani Papa Penedict wa 16 anatazamiwa kutembelea utawala ghasibu wa Israel na Ukanda wa Gaza tarehe 16 Mei mwaka huu. Safari hiyo imepingwa na makundi mbalimbali ya Kiislamu na Kikristo ya Palestina. 387842

captcha