IQNA

16:11 - April 14, 2009
Habari ID: 1764951

Kuzuru haram za mawalii wa Mwenyezi Mungu kunamuelekeza mja kwa Mola wake

Hujjatul Islam Walmuslimin Murtadha Agha Tehrani amesisitiza juu ya udharura wa kuimarishwa imani ya mwanadamu na kuongeza kuwa kuzuru haram za mawalii wa Mwenyezi Mungu kunamuelekeza mja kwa Mola wake Muumba.

Sheikh Agha Tehrani ambaye pia ni mbenge katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema katika mji mtakatifu wa Madina kwamba, kama ambavyo mwanadamu anahitajia chakula, mazoezi ya viungo na mapumziko kwa ajili ya kuimarisha mwili wake, vilevile anahitajia kuimarisha roho yake kwa chakula cha kiroho kama kuzuru haram za mawalii wa Mwenyezi Mungu. Ameongeza kuwa mwanadamu hawezi kuishi bila ya kupata maji na chakula na kwamba roho yake pia hufariki dunia na kufa iwapo haitapata chakula cha kutosha cha kiroho.
Sheikh Tehrani amesisitiza kuwa kuzuru haram za mawalii wa Mwenyezi Mungu na kumuomba dua Mola Muumba humkurubisha mwanadamu katika ukamilifu ambao haufikii kiwango chake cha juu bila ya kuwa karibu na Ahlubaiti wa Mtume Muhammad (saw).387259


captcha