IQNA

11:56 - April 15, 2009
Habari ID: 1765255

Mkutano wa kimataifa wa Utafiti wa Sheria za Kiislamu kufanyika nchini Malaysia

Mkutano wa kimataifa wa Utafiti wa Sheria za Kiislamu umepangwa kufanyika tarehe 15 na 16 Julai nchini Malaysia.

Lengo la mkutano huo limetajwa kuwa ni kuzidisha ushirikiano wa kielimu kati ya taasisi za utafiti, kuasisi kanali za kielimu na kiutafiti katika uga wa kimataifa na kubaini changamoto zinazokabili tafiti mbalimbali katika sheria za Kiislamu.
Masuala mengine yatakayojadiliwa katika mkutano huo ni elimu na malezi katika sheria za Kiislamu, sheria za Kiislamu na jamii ya sasa, utajiri wa Waislamu na uendeshaji wa rasilimali, sheria za Kiislamu na tamaduni mbalimbali, sheria za uwekezaji wa Kiislamu na kadhalika. 388324

captcha