IQNA

12:16 - April 16, 2009
Habari ID: 1765618

Mazungumzo ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ya Palestina kuanza

Mmoja wa viongozi wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas ametangaza kuwa mazungumzo kati ya harakati hiyo na chama cha Fat'h ya kufikia mapatano ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ya Palestina yataanza hivi karibuni mjini Cairo.

Kwa mujibu wa Gazati la ArabNews, Sami Abu Zuhri amewaambia waandishi habari kwamba mazungumzo hayo yataanza tarehe 26 Aprili. Amekitaka chama cha Fat'h kushiriki kwa nia njema katika mazungumzo hayo na kukoma kuwatia mbaroni wanachama wa Hamas. Inasemekana kwamba vyama hivyo viwili vimeafikiana kuhusiana na suala la kubuni serikali ya umoja wa kitaifa na kufanyika uchaguzi mkuu ifikapo mwezi Januari 2010 lakini mazungumzo yao hivi sasa yanahusiana na sheria mpya za uchaguzi zinazopaswa kutekelezwa ili kuhakikisha kwamba uchaguzi huo unafanyika kwa uhuru na haki kamili.
Hamas imesema wazi kwamba inapinga kufanyika kwa uchaguzi huo katika misingi na masharti yaliyotolewa na Kamati ya Pande Nne, yaani Marekani, Russia, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya ambayo inaitaka Hamas kuutambua rasmi utawala haramu wa Israel na kukubali kusimamisha mapambano ya jihadi dhidi ya ukaliwaji haramu wa ardhi za Wapalestina.389040
captcha