IQNA

9:36 - April 18, 2009
Habari ID: 1765982

Usajili wa majina ya washiriki wa mashindano ya 19 ya kuhifadhi Qur'ani ya Sultan Qabus

Taasisi ya Kiutamaduni ya Sultan Qabus ya nchini Oman imeanza kusajili majina ya watu walio na hamu ya kushiriki katika duru ya 19 ya mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu ya Sultan Qabus.

Taasisi hiyo metangaza kuwa, sharti la kushiriki katika mashindano hayo ni kuwa na uraia wa Oman. Imeongeza kuwa, kutokuwa mashuhuri kwa wasomaji na vilevile kutoshinda zawadi za kimataifa na kitaifa za usomaji na uhifadhi wa Qur'ani ni masharti mengine ya kushiriki katika mashindano hayo.
Mashindano hayo yatafanyika kwa utaratibi ufuatao; kuhifadhi Qur'ani nzima, juzuu 24, juzuu 18 uzuu 12 na juzuu 6 ambapo zote zitatakiwa kuhifadhiwa kwa mbinu ya tajweed.
Washiriki wanapasa kuwa wamesajili majina yao kufikia tarehe 26 Juni katika misikiti ya Ijumaa ya Sultan Qabus kote nchini humo. Utangulizi wa mashindano hayo utazinduliwa tarehe 4 Julai na mashindano yenyewe kumalizika tarehe18 Julai. 389123
captcha