IQNA

16:31 - April 19, 2009
Habari ID: 1766964

Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi lalaani jinai za Wazayuni

Jumuiya ya Mawakili wa Kiarabu na Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi (CCG) zimelaani hatua za kupindukia mipaka na kijinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya taifa la Palestina.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Syria SANA, jumuiya hiyo ya mawakili wa Kiarabu imelaani vitendo vya uharibifu vinavyotekelezwa na utawala haramu wa Israel huko katika mji wa Beitul Muqaddas na kusema kuwa lengo la mwisho la utawala huo ni kuharibu kabisa Msikiti wa al-Aqsa.
Jumuiya hiyo imetoa taarifa ikisema kuwa hatua za utawala wa Kizayuni ya kuvuruga muundo wa kijamii katika mji huo ambao una utambulisho wa Kiislamu na Kiarabu ni jambo linalokiuka wazi sheria na maazimio ya kimataifa na kuyataka mashirika pamoja na taasisi zote za kimatifa kuchukua hatua za haraka katika kukabilia na siasa hizo haribifu.
Jumuiya ya Mawakili wa Kirabu pia imelitaka Shrika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa kubuni kamisheni ya kuchunguza ukiukaji huo wa utawala haramu wa Israel na pia kulitaka Baraza la Usalama la umoja huo kuchukua hatua za dharura kwa lengo la kusimamisha ukiukaji huo wa wazi wa Israel dhidi ya matukufu ya Kiislamu na haki za Waarabu.
Katika taarifa hiyo, Abdulrahman bin Hamad al-Atiyya, Katibu Mkuu wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi ameitaka jamii ya kimataifa kutekeleza ipaswavyo majukumu yake na kukomesha hujuma na jinai za Israel dhidi ya taifa la Palestina, jambo ambalo limehatarisha usalama na amani ya eneo zima la Mashariki ya Kati. Al-Atiyya pia amesisitiza juu ya uungaji mkono wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi kwa taifa la Palestina hadi kuthibiti na kurudishwa haki zake zote ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa taifa huru la Palestina, mji mkuu wake ukiwa ni Quds Tukufu. 390497
captcha