Hayo yamesemwa na Muhammad Asad mwanafikra na msomi wa Lebanon katika mazungumzo yake na Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani IQNA. Ameongeza kuwa hii leo umuhimu wa kufanyika ubunifu huo kuhusiana na masuala ya kidini, na hasa katika masuala ya kiutamaduni, kielimu na kiuchumi unahisika zaidi kuliko wakati mwingine wowote.
Huku akisema kuwa kutolewa kwa mitazamo mipya ya kielimu kuhusiana na sheria za kidini kunaweza kuleta msisimuko na ubunifu kuhusiana na suala hilo, mwanafikra huyo wa Lebanon amesema kuwa ubunifu katika masuala ya kidini na upashaji habari sahihi katika uwanja huo ni jambo linaloweza kuwapa Waislamu uwezo wa kukabiliana na njama za maadui wa Uislamu wa nchi za Magharibi.
Muhammad Asad ameashiria nafasi ya Imam Khomeni (MA) katika kuleta fikra mpya za kuhuisha Uislamu na kusema kuwa Imam Khomeini aliongoza na kuwaelekeza Waislamu katika mafundisho sahihi ya Kiislamu na hivyo kuleta muamko mpya katika mitazamo na fikra za kidini kwa maslahi ya umma mzima wa Kiislamu.
Huku akisisitiza udharura wa kutazamwa upya baadhi ya fikra na mitazamo isiyooana na ukweli wa mambo katika maisha ya wanadamu, msomi Asad amesisitiza kwamba ubunifu na fikra mpya katika Uislamu zinapasa kushughulikiwa kwa msingi wa mafundisho halisi ya Kiislamu na hasa katika kulifahamisha tabaka la vijana na wanachuo Uislamu halisi. 390228