Ekmeleddin Ihsanoglu, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC amesema kwamba, jumuiya hiyo ina mpango wa kuandaa kikao cha kimataifa kwa lengo la kuchunguza mgogoro wa kifedha duniani na pia mfumo wa benki za Kiislamu.
Akizungumza katika kikao cha 32 cha Kamati ya Kiislamu Kuhusu Masuala ya Kiuchumi huko mjini Jiddah nchini Saudi Arabia, Ihsanoglu amesema kuwa mgogoro wa kiuchumi na kifedha duniani umeitia wasiwasi mkubwa jumuiya ya OIC na nchi zote za Kiislamu kwa ujumla. Ameongeza kuwa umoja huo umekuwa ukishirikiana na mashirika ya kimataifa na nchi mbalimbali duniani kwa lengo la kutekeleza mipango ya pamoja ya kiuchumi ili kukabiliana na mgogoro huo wa kifedha ambao imeziathiri nchi nyingi duniani.
Huku akisisitiza udharura wa kutatuliwa kitaalamu mgogoro wa hivi sasa wa kiuchumi na nchi wanachama wa OIC, al-Tuwaijri amesema kuwa sifa bora ya nchi za Kiislamu ni thamani yao ya kistratejia kwa sababu ulimwengu wa Kiislamu unaunda sudusi moja ya eneo zima la dunia na thumuni moja ya jamii yote ya wanadamu ulimwenguni. 391459