IQNA

10:39 - April 25, 2009
Habari ID: 1769265

Vatican na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu zatia saini mkataba wa ushirikiano

Maafisa wa Vatican na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu wametia saini makubaliano ya ushirikiano wa pande mbili katika masuala ya kisiasa na kiutamaduni.

Shirika la habari la Ufaransa (AFP) limeripoti kuwa mkataba huo umetiwa saini kati ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Amr Mussa na Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Vatican Dominique Memberti kwa shabaha ya kustawisha uhusiano na kuimarisha amani ya kieneo na kimataifa.
Taarifa iliyotolewa na Vatican imesema kuwa mkataba huo unaweza kusaidia juhudi za kuimarisha uhusiano kati ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Vatican katika masuala ya kisiasa na kiutamaduni na kustawisha amani ya kieneo.
Mkataba huo pia inasisitiza juu ya kuitishwa vikao na makongamano ya kidini kati ya pande hizo mbili.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Amr Mussa pia jana Ijumaa alionana na kufanya mazungumzo na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Benedict wa 16. 393526


captcha