IQNA

0:38 - May 01, 2009
Habari ID: 1772097

Mkutano wa kumuenzi Mtume wa Uislamu wafanyika London

Mkutano wa kumuenzi Mtume Muhammad (saw) umefanyika katika Kituo cha Utamaduni cha Friends House mjini London chini ya usimamizi wa Jumuiya ya Vijana ya Anatoli.

Mkutano huo ambao umehudhuriwa na maulamaa, waandishi na Waislamu Waturuki wanaoishi Uingereza, umefunguliwa kwa kisomo cha Qur'ani kilichosomwa kwa pamoja na hadhirina wote. Mwandishi Rashid Hayalmaz amehutubia mkutano huo na kusema kuwa Mtume Muhammad (saw) alifanya kazi kubwa ya muujiza ya kueneza Uislamu na kwamba watu wengi walikubali dini hiyo kwa kuathirika na mwenendo na tabia nzuri za mtukufu huyo.
Hayalmaz amesema kuwa hata wakati alipokuwa akienda kupigana vita na kaumu fulani, Mtume Muhammad (saw) alikuwa kwanza akiwaombea dua kwa Mwenyezi Mungu ili awaongoze watu hao na hakuamiliana na mtu yeyote kwa mwenendo mbaya.
Sambamba na mkutano huo kulikuwepo na ratiba mbalimbali za kiutamaduni, nyimbo na mashairi ya kumsifu Mtume na masahaba zake. 396750



captcha