IQNA

Malaysia, mwenyeji wa kikao cha kwanza cha wanawake wa nchi za Kiislamu

9:30 - May 06, 2009
Habari ID: 1774568
Maonyesho na kikao cha kwanza cha wanawake wa nchi za Kiislamu kitafanyika tarehe 28 hadi 31 za mwezi huu wa Mei huu huko Kuala Lumpur Malaysia.
Kwa mujibu wa tovuti ya Trade Chakra, lengo la kufanyika maonyesho na kikao hicho ni kunyanyua nafasi ya kiuchumi na kijamii ya wanawake wa Kiislamu pamoja na kuinua nafasi yao katika ustawi wa jamii, kuimarisha uelewa wao kuhusiana na matatizo ya kijamii na kiuchumi ya wanawake, kuimarisha mtandao wa mawasiliano kati ya wanawake wa Kiislamu na kuimarisha mawasiliano hayo katika nyanja za kibiashara.
Malengo mengine ya kuandaliwa maonyesho na kikao hicho cha Malaysia ni kuandaa mazingira yanayofaa ya biashara kwa wanawake wajasiriamali wa Kiislamu kwa shabaha ya kugundua nyanja mpya za kibiashara na ubadilishanaji habari na uzoefu katika uwanja wa biashara.
Wakurugenzi, maafisa wa serikali, wauzaji na waagizaji wa bidhaa kutoka nje, wafanyabiashara, wakuu wa ofisi za biashara na jumuia za biashara za wanawake wa nchi za Kiislamu ni miongoni mwa watu walioalikwa kushiriki katika maonyesho na kikao hicho. 399716
captcha