IQNA

Kongamano kuhusu Bibi Fatima Zahra (AS) katika bunge la Uingereza

12:30 - May 12, 2009
Habari ID: 1777353
Kongamano la Kimataifa lenye anuani ya, 'Fatima Zahra (AS) Mwanamke mwenye Nuru' linafanyika Jumanne katika Baraza la Malodi nchini Uingereza.
Kongamano hilo linaandaliwa na Baraza la Imam Hussein (AS) kwa lengo la kumuarifisha binti wa Mtume (SAW) kama kigezo katika kueneza maelewano baina ya dini na madhehebu mbali mbali pamoja na kumuarifisha kama mwanamke wa heshima ya juu katika Uislamu. Kongamano hilo aidha linaloenga kuonyesha nafasi muhimu ya wanawake katika historia ya Uislamu.
Hii ndio mara ya kwanza hafla kama hiyo inaandaliwa bunge la Uingereza kupitia ushirikiano wa Lodi Nazeer Ahmad. Mwenyekiti wa Baraza la Imam Hussein (AS) Wakili Rubab Mehdi amesema kongamano hilo la kumenzi Bibi Fatima (AS) ni la aina yake ni linafanyika na litatoa fursa ya mazungmzo baina ya Waislamu na viongozi wa ngazi za juu wa kisiasa nchini Uingereza. Amesema hiyo itakuwa pia fursa ya kubunia uhusiano wa kudumu kati ya Waislamu watunga sheria na vyombo vya habari. Bi.Mehdi amesema ni muhimu kwa Waislamu kutangulia kuwaelimisha wasio kuwa Waislamu kuhusu Uislamu na Waisalmu ili kuleta maelewano na mahusiano mazuri katika jamii. 403477

captcha