IQNA

14:18 - May 16, 2009
Habari ID: 1778916

Papa achukue hatua za kivitendo kuzuia kuharibiwa athari za kidini Quds

Baraza la Kiislamu na Kikristo la kuutetea Mji wa Quds na Msikiti wa Al Aqsa limemtaka Papa Benedict XVI kiongozi wa kanisa Katoliki duniani kuchukua hatua za kivitendo kusitisha hujuma haribifu ya Wazayuni dhidi ya Quds Tukufu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Hassan Khatar Katibu Mkuu wa Baraza la Kiislamu na Kikristo la kuutetea Mji wa Quds na Msikiti wa Al Aqsa Ijumaa akihutubu huko Ramallah katika kikao kilichofanyika Kwa mnasaba wa mwaka wa 61 wa siku ya kuasisiwa utawala haramu wa Israel katika ardhi zlizoghusubiwa za Palestina, siku ambayo ni maarufu kwa jina la Nakba au maafa makuu, amemtaka Papa kuchukua hatua za kivitendo na imara kuhitimisha masaibu na matatizo ya Wapalestina ambayo yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya miongo sita.
Akihutubu katika kikao hicho ambacho pia kilihudhuriwa na Sheikh Taysir al Tamimi Kadhi Mkuu wa Palestina pamoja na viongozi na wasomi Wakristo na Waislamu, Hassan Khatar amesema: "Papa Benedict XVI katika safari yake Quds Tukufu alishuhudia uharibifu unaotelekezwa na Wazayuni dhidi ya Quds Tukufu, Msikiti wa Al Aqsa pamoja na matukufu mengine ya Kiislamu na Kikristo.
Washiriki katika kikao hicho wametoa taarifa na kulaani hatua za jeshi la Israel linalotekeleza sera za ukandamizaji na ubaguzi dhidi ya Wapalestina wakati wa safari ya Papa katika mji wa Quds. Wamesema mzingiro wa wanajeshi hao wa Kizayuni huko Quds umepelekea Waislamu kutoweza kusali katika Msikiti wa Al Aqsa jambo ambalo ni dhihirisho la utambulisho wa kibaguzi wa utawala haramu wa Israel. 405378
captcha