IQNA

17:01 - May 16, 2009
Habari ID: 1779038

Mashindano ya kuhifadhi maneno ya Hekima ya Nahjul Balagha kwa wanafunzi wa kigeni nchini Iran

Mashindano ya kiutamaduni na Kiislamu ya kuhifadhi maneno na ibara za hekima katika Nahjul Balagha kwa wanafunzi wa kigeni nchini Iran yameandaliwa na Taasisi ya Fikra za Kiislamu ya nchini Pakistan.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IQNA, lengo la kufanyika mashindano hayo ni kuwafahamisha zaidi wanafunzi mafundisho ya Imam Ali (as), kunyanyua uwezo wa kuhubiri na kushiriki katika kueneza maarifa na mafundisho ya Nahjul Balagha. Mashindano hayo ambayo yamepangwa kufanyika tarehe 31 Mei yamepangwa kufanyika kwa wakati mmoja katika vyuo vinne vya Imam Khomeini, Hujjatiyya, Bintul Huda na Az-Zahra (as). Mashindano hayo yamekaribishwa sana na wanafunzi wa kigeni na hadi sasa wanafunzi 1000 tayari wamesajili majina yao kwa lengo la kushiriki katika mchuano wa kuhifadhi maneno hayo ya hekima ya Imam Ali (as). 405492
captcha