IQNA

Wizara ya Waqfu Malaysia ina nafasi muhimu katika mwamko wa Kiislamu

10:21 - May 17, 2009
Habari ID: 1779265
Waziri wa Masuala ya Waqfu na Kiislamu nchini Malaysia Jamil Kheir Bin Haj Bahrum amesema wizara yake ina nafasi muhimu katika kuleta mwamko miongoni mwa Waislamu.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA Kusini-Mashariki mwa Asia, Jamil Kheir Bin Haj Bahrum ameongeza kuwa: ‘Ushirikiano miongoni mwa vitengo husika katika idara ya Waqfu kwa usimamizi wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC ni jambo muhimu sana na kunahitajika juhudi zaidi za uwekezaji katika idara ya Waqfu ili kulinda maslahi ya jamii ya Kiislamu’.
Waziri huyo wa masuala ya Kiislamu Malaysia amesema Waqfu ulikuwa na nafasi muhimu katika mwamko wa Ummah wa Kiislamu na taasisi hii ya Kiislamu ingali inaendeleza harakati zake ambazo sasa zimeongezeka zaidi ya huko nyuma. 405779






captcha