IQNA

17:01 - June 06, 2009
Habari ID: 1787835

Maadui wanapanga njama dhidi ya mfumo wa Kiislamu kwa kuvuruga uchaguzi

Khatibu wa sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema kuwa, hitilafu iliyopo kati ya Jamhuri ya Kiislamu na Marekani inatokana na hatua ya Washington ya kuunga mkono kibubusa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Khatibu wa sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema kuwa, hitilafu iliyopo kati ya Jamhuri ya Kiislamu na Marekani inatokana na hatua ya Washington ya kuunga mkono kibubusa utawala wa Kizayuni wa Israel. Akizungumza kwenye khutba za sala ya Ijumaa mbele ya hadhara kubwa kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Tehran, Ayatullah Ahmad Jannati amezungumzia matamshi yaliyotolewa jana na Rais Barack Obama wa Marekani mjini Cairo na kuongeza kuwa, hitilafu kati ya pande mbili inatokana na masuala mawili muhimu, moja likiwa uungaji mkono wa Marekani kwa utawala wa Israel ambao unatekeleza shari, dhulma,ukandamizaji na mauaji katika eneo la Mashariki ya Kati. Ayatullah Jannati ameongeza kuwa, iwapo Marekani inataka kuendelea kuunga mkono Israel, uhusiano wa Tehran na Washington utaendelea kubaki hivihivi. Ameongeza kuwa, uingiliaji kati katika masuala ya Lebanon, Palestina, Afghanistan na Iraq ni miongoni mwa masuala mengine ambayo Washington inapaswa kuepukana nayo na kuongeza kuwa, kuendelea kuchukiwa Marekani hakuwezi kuondoka kwa kuletwa nara za mabadiliko. Katibu wa Baraza la Kulinda Katiba amesema kwenye khutba za sala ya Ijumaa kuhusiana na siku ya kuadhimisha harakati ya 15 Khordad ya mwaka 1342 Hijria Shamsia na kueleza kwamba harakati hiyo iliandaa mazingira ya mapinduzi ya Kiislamu nchini na kuongeza kuwa, mapinduzi ya Kiislamu yaliyoongozwa na Hayati Imam Khomeini MA hayana mfano katika historia ya mwanadamu, kwani hayakutegemea mashariki wala magharibi, bali ni kumkomboa mwanadamu na kuwapatia izza na heshima wananchi wa Iran. Akizungumzia propaganda chafu zinazotolewa na vyombo vya habari vya magharibi kuhusiana na uchaguzi wa rais utakaofanyika wiki ijayo, Ayatullah Jannati amesisitiza kuwa, malengo ya maadui wala siyo uchaguzi wa Iran, bali malengo yao ni kuzusha fitna na mifarakano na hatimaye kuusambaratisha mfumo na mapinduzi ya Kiislamu, amma wananchi wa Iran wako macho na bila shaka watazima njama hizo kutokana na kufuata kikamilifu miongozo makini ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
416287
captcha