Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Baraza la Ushirikiano wa Kiislamu la Marekani aidha limetoa wito kwa Waislamu na Wamarekani wote kuwalaani wenye chuki dhidi ya Uislamu wanaopinga ujenzi wa kituo cha Kiislamu mjini New York.
Nahad Awad Mkuu wa Kamati ya Utendaji ya Baraza la Ushirikiano wa Kiislamu la Marekani amesema: “Watu wenye taasubu na misimamo mikali hawapaswi kuwa kizingiti katika ujenzi wa kituo cha Kiislamu mjini New York”.
Awad ameongeza kuwa kuibuka wimbi jipya la wanaopinga ujenzi wa misikiti na vituo vya Kiislamu ni jambo linaloashiria kuenea chuki dhidi ya Uislamu nchini Marekani.
626059