IQNA

19:10 - August 10, 2010
Habari ID: 1970918

Kuanza mashindano ya kimataifa ya elektroniki, maalumu kwa mwezi wa Ramadhani nchini Kuwait

Mashindano ya kimataifa ya elektroniki maalumu kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani yameanza leo Jumanne nchini Kuwait.

Mashindano hayo ambayo yataendelea hadi Alkhamisi tarehe 12 Agosti yameandaliwa na Idara ya Utamaduni wa Kiislamu ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Kuwait.
Kuhusu mashindano hayo gazeti la Kuwait la al-Anbaa limemnukuu Falah al-Ajmi, mkuu wa kitengo cha masuala ya vyombo vya habari cha wizara hiyo akisema kuwa walio na hamu ya kushiriki katika mashindano hayo wanaweza kushiriki kwa kutumia anwani ifuatayo ya tovuti ya Wizara ya Wakfu na masuala ya Kiislamu ya Kuwait: www.islam.gov.kw/thaqafa.
Amesema wanaweza kushiriki katika mashindano hayo kwa kujibu maswali ya utafiti wa dini na fikhi ya Kiislamu yaliyowekwa katika kurasa za tovuti hiyo. Ameendelea kusema kuwa dinari 1,500 zitatolewa na Wizara ya Wakfu ya Kuwait kwa washindi 150 wa mashindano hayo. Amesema, mashindano hayo yanafanyika katika fremu ya shughuli za wizara hiyo katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. 630409
captcha