Kituo hicho kitasimamiwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Utambuzi wa Uislamu (WAI) iliyo chini ya Taasisi ya Kimataifa ya Uislamu.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Uislamu mjini Makka Sheikh Ahmad al Shamrani amesema kuwa walinganiaji watakapokelewa katika kituo hicho watapewa mafunzo ya dharura ya Qur'ani na Suna za Mtume (swa).
Ameongeza kuwa walinganiaji hao watapewa mafunzo ya mbinu za kuhubiri na kuutambulisha vyema Uislamu katika nchi mbalimbali.
Ahmad al Shamrani amesema lengo la kuanzishwa kituo hicho ni kutayarisha watu wenye sifa zinazohitajika kwa ajili ya kuarifisha Uislamu katika nchi mbalimbali kupitia njia ya kuanzisha vituo vya kulingania Uislamu katika nchi tofauti na kuanzisha mitandao ya mawasiliano na vituo na taasisi nyingine za Kiislamu.
Jumuiya ya Kimataifa ya Utambuzi wa Uislamu (WAI) ni taasisi isiyokuwa ya serikali ambayo makao yake makuu yako katika mji mtakatifu wa Madina na ina ofisi katika miji ya Riyadh, Makka na Jiddah nchini Saudi Arabia. 631049