IQNA

Utafiti kuhusu satalaiti ya Kiislamu ya kutafuta hilali wamalizika

18:54 - August 16, 2010
Habari ID: 1974872
Utafiti wa kisayansi na kisheria kuhusu utengenezaji wa satalaiti ya Kiislamu kwa ajili ya kutafuta hilali kwa lengo la kuleta umoja kuhusu suala la kuanza na kumalizika miezi ya hijria qamaria umemalizika nchini Misri.
Kwa mujibu wa tovuti ya Idhaa ya Kiarabu ya Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB (arabic.irib.ir), Kituo cha Utafiti wa Anga za Mbali cha Chuo Kikuu cha Cairo kimetoa tangazo kuhusu mpango wa kuanzishwa satalaiti ya Kiislamu na kusema satalaiti hii itatengenezwa na shirika moja la kitaalamu la Italia na baadhi ya vipuri vitatengenezewa Misri.
Kituo cha Utafiti wa Anga za Mbali cha Chuo Kikuu cha Cairo kimesema satalaiti hiyo itakuwa na uwezo wa kuainisha wakati wa kuanza miezi ya hijria qamaria, kuainisha kibala katika maeneo mbali mbali duniani, kuainisha wakati wa sala hasa katika maeneo ya mbali na vile vile kupima viwango vya uharibifu wa hewa.
Chuo hicho cha Misri kimetoa wito wa uwekezaji wa nchi za Kiislamu katika ujenzi wa satalaiti hiyo.
634437
captcha