Mashindano hayo yaliyoanza tarehe 9 ya mwezi wa Ramadhani yaliandaliwa na Tasisi ya Qur'ani ya al-Iraqiyya katika mji wa Kadhimein na yamemalizika kwa kutuzwa washindi wa mashindano hayo. Mashindano yaliyotajwa yaliwajumuisha wasomaji Qur'ani kutoka mikoa mbalimbali ya Iraq. Mwishoni mwa sherehe za kuhitimisha mashindano hayo, Farajullah Shadhili, refa mashuhuri wa kimataifa wa Qur'ani alimtembelea Rafi' al-Aamiri mkuu wa Taasisi ya Qur'ani ya al-Iraqiyya na wasimamizi kadhaa wa taasisi hiyo na kuwatakia funga njema ya mwezi mtukufu wa Ramadhani pamoja na wananchi wote wa Iraq. Vilevile ameishukuru Taasisi ya Qur'ani ya al-Iraqiyya kutokana na shughuli zake za kuhudumia Qur'ani Tukufu pamoja na kuandaa mashindano ya usomaji wa kitabu hiki kitakatifu. 639937