Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA nchini Uturuki, timu ya wakaguzi hao itawahoji raia wa Uturuki walioshuhudia hujuma hiyo ya kinyama iliyotekelezwa na vikosi vya Wazayuni katika maji ya kimataifa.
Itakumbukwa kuwa katika hujuma hiyo ya maharamia wa kiserikali wa utawwala wa Kizayuni wa Israel, wanaharakati tisa wa Uturuki waliuawa shahidi na makumi ya wengine kujeruhiwa. Aidha maharamia hao wa jeshi la wanamaji la utawala haramu wa Israeli walipora mali binafasi za wanaharakati hao wa haki za binadamu waliokuwa wakiwapelekea misaada Wapalestina wanaokabiliwa na mzingiro katika Ukanda wa Ghaza.
640754