Cairo mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa "Mazungmzo ya Uislamu na Ukristo"
Kongamano la tatu la pamoja baina ya Jumuiya ya Vyuo Vikuu vya Kiislamu na Chuo Kikuu Huria cha Amsterdam Uholanzi chini ya anuani ya "Mazungmzo ya Uislamu na Ukristo" itafanyika kuanzia tarehe 22-24 Novemba mwaka huu katika mji mkuu wa Misri Cairo.
Kwa mujibu wa Ja'afar Abdulsalam Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vyuo Vikuu vya Kiislamu, kongamano hilo litahudhuriwa na zaidi ya wasomi 100 Waislamu na Wakristo kutoka sehemu mbali mbali duniani.
Ameongeza kuwa: "Mada kuu ya kongamano la Cairo itakuwa ni "Umoja au Upweke wa Mwenyezi Mungu" nayo mada ya pili itakuwa, "Mafunzo ya Kiislamu katika Ulimwengu wa Magharibi".
643167