Kikao hicho kitafanyika chini ya anwani ya 'Dini na Maisha, Mazungumzo ya Ukristo na Uislamu'. Kwa mujibu wa tovuti ya Muhit, Jaafar Abdu Salaam, mkuu wa umoja uliotajwa wa vyuo vya Kiislamu amesema kuhusu jambo hilo kwamba zaidi ya wasomi na wanafikra wa Kiislamu na Kikristo 100 kutoka nchi mbalimbali za dunia watashiriki katika kikao hicho. Amesema 'Kumpwekesha Mwenyezi Mungu' itakuwa maudhui ya kwanza muhimu ya kikao hicho ambapo washiriki watapata fursa ya kutoa mitazamo yao kuhusiana na sifa za Mwenyezi Mungu. Maudhui ya pili itahusu mafundisho ya Kiislamu katika nchi za Magharibi. Mbinu za mafunzo na utafiti wa Kiislamu katika jamii za Magharibi zitatathminiwa na makala mbalimbali kuhusu Uislamu katika nchi za Magharibi kuwasilishwa.
Abdu Salaam amemaliza kwa kusema kuwa maadili ya kitiba katika mtazamo wa Uislamu na Ukristo ni maudhui nyingine itakayojadiliwa katika kikao hicho cha siku nne. 643167