IQNA

Mji wa Najaf al Ashraf wajitayarisha kwa ajili ya wanaozuru haram ya Imam Ali (as)

2:58 - August 30, 2010
Habari ID: 1983955
Wizara ya Afya ya Iraq imezitaka jumuiya za masuala ya afya za miji mitakatifu ya Karbala na Najaf kujitayarisha kwa ajili ya maombolezo ya kukumbuka siku ya kuuawa shahidi Imam Ali bin Abi Twalib (as).
Mkuu wa kitengo cha operesheni za masuala ya tiba na huduma cha Wizara ya Afya ya Iraq Dakta Jasib Latif Ali amewaambia waandishi habari kwamba wizara hiyo inajitayarisha kwa ajili ya shughuli ya maombolezo ya kukumbuka siku ya kuuawa shahidi Imam Ali (as) inayosadifiana na tarehe 21 mwezi wa Ramadhami na imetayarisha vituo makhsusi vya afya katika mikoa ya Najaf, Karbala na mikoa jirani.
Ameongeza kuwa vituo hivyo vya afya vimeboresha kiwango cha huduma za kiafya na kudhamini akiba ya dawa na suhula nyingine za kitiba.
Latif Ali amewataka watu wanaozuru maeneo hayo matakatifu hususan watoto wadogo kujiepusha na vyakula au vinywaji visivyokuwa na kiwango kinachotakikana cha afya kwa ajili ya kulinda afya zao. 644344
captcha