Kwa mujibu wa gazeti la Tennessean Makasisi Bob Old na Denny Allan ambao hawafungamani na makanisa yoyote muhimu ya Marekani walichoma tarjuma hizo za Qur'ani licha ya kuwepo upinzani mkali wa makanisa muhimu ya Marekani dhidi ya jambo hilo hatari. Makasisi hao walichoma tarjuma hiyo ya Qur'ani katika uwanja wa nyumba ya Kasisi Bob Old huko katika mji wa Springfield.
Baada ya kuchoma moto kitabu hicho, Bob Old alizungumza akidai kuwa Qur'ani ni kitabu kinachochukiza, kilichojaa uongo na kumtaja Mtume Mtukufu Muhammad (saw) kuwa ni mtume wa uongo. Wamesema wamechukua hatua ya kukichoma moto kitabu hicho kama jibu la ujumbe waliotakiwa kuutekeleza na mungu wao!
Kwa mujibu wa shirika la habari la Zeenews, hatua kama hiyo ya dharau dhidi ya Qur'ani Tukufu ilichukuliwa na mmoja wa washiriki wa kumbukumbu ya kuadhimisha matukio ya Septemba 11 nchini Marekani ambaye alichoa moto kurasa kadhaa za Qur'ani baada ya kuzichanachana.
Vileviel mtu mwingine huko New York alichana kurasa za Qur'ani na kufanya vitendo vya aibu na kurasa hizo, jambo ambalo limeshangaza na kuwakasirisha wengi duniani.
Mambo hayo yote ya dharau na ubezaji dhidi ya Qur'ani Tukufu na Waislamu yanatekelezwa nchini Marekani hali ya kuwa watawala wa nchi hiyo wamekaa kimya bila kuchukua hatua yoyote ya kisheria dhidi ya wahalifu hao. Hayo yote yanafanyika kwa kisingizio cha uhuru wa kusema na kujieleza.
Kasisi Terry Jones wa Kanisa dogo la Dove World Outreach Center katika jimbo la Florida siku ya Ijumaa alitakangaza kufutilia mbali mpango wake wa awali wa kutaka kuichomo moto Qur'ani Tukufu kwa mnasaba wa Setpemba 11 kutokana na mashinikizo makubwa ya Waislamu yaliyotolewa katika ngazi za kimataifa. Wiki kadhaa kabla ya tarehe hiyo, alitangaza siku hiyo kuwa ni 'siku ya kimataifa ya kuchoma Qur'ani' na hivyo kuamsha hasira kali za Waislamu duniani.
Dharu hiyo haikuwakera Waislamu tu bali hata Wakristo wapenda haki duniani. Ni wazi kuwa kitendo chake hicho kimewachochea watu wengine walio na misimamo ya chuki na ubaguzi kama yeye kuchukua hatua ya kuchoma na kuchana Qur'ani nchini Marekani.
Kwa kuzingatia hali hiyo ya kusikitisha na kuongezeka wimbi la dharau dhidi ya matukufu ya Kiislamu nchini Marekani, Waislamu na wapenda haki wote duniani wanapasa kulaani vikali vitendo hivyo vya dharau na kusisitiza kuwa hivyo ni vitendo vinavyokwenda kinyume kabisa na misingi ya maadili ya kibinadamu. Wanapasa kutilia mkazo nukta hii kwamba, jamii ya kimataifa haikubaliani na suala hilo na kwamba mtu yoyote atakayekariri kitendo hicho cha dharau atachukuliwa hatua kali za kisheria. 652952