Kwa mujibu wa tovuti ya Calgary Herald, Terry Taylor amezungumzia suala hilo hivi karibuni katika kikao cha kutetea Qur'ani Tukufu kilichandaliwa maalumu kwa ajili ya kulalamikia kitendo cha uchomaji moto Qur'ani Tukufu nchini Marekani.
Washiriki wa kikao hicho kilichoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu wa Canada huko katika mji wa Calgary, wamelaani kitendo cha dharau dhidi ya Qur'ani na kuzitaka jumuiya zote za kidini duniani kushirikiana katika kulaani vitendo kama hivyo.
Sayyid Suhrevardi, mratibu wa kikao hicho amesema kuwa lengo la kuandaliwa kikao hicho ni kuwathibitishia watu kwamba kitabu cha Qur'ani ni kitakatifu kama vilivyo vitabu vingine vya mbinguni ikiwemo injili.
Katika upande mwingine makanisa ya mji wa Louisville katika jimbo la Kentucky nchini Marekani yameandaa maonyesho ya vitabu vitakatifu vya dini mbalimbali, ikiwemo Qur'ani Tukufu. 653035